RafikiElimu FOUNDATION ni Taasisi Isiyokuwa ya Kiserikali ( NGO ) inayo jihusisha na maendeleo ya jamii. tAASISI kupitia mradi wake " Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini " ( EUMIVI- Project ) inapenda kuwatangazia wakaazi wote wa jijini Dar Es salaam, nafasi za mafunzo ya ujasiriamali. Mafunzo yatakayo tolewa ni pamoja na :
1. Utengenezaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kama vile Sabuni Za Aina Zote, Batiki, Chaki, Mishumaa, Batiki na Usindikaji,
2. Elimu ya ujasiriamali
3. Sheria za biashara,
4. Usimamizi na uongozi wa biashara
5. Usimamizi wa miradi,,
6. uwekaji na ukopaji nakadhalika.
Washiriki wa mafunzo watawekwa katika vikundi vya maendeleo ya jamii vya watu 20 kila kikundi na wataunganishwa katika Mtandao Wa Vikundi Vya Maendeleo Ya Jamii Tanzania, ambao upo chini ya asasi ya RafikiElimu Foundation.
Mafunzo yataanza kutolewa tarehe 01 Novemba 2012.
Tarehe Ya Kuanza Kujiandikisha ni tarehe 08 OKTOBA 2012.
Mwisho wa kujiandikisha katika mafunzo haya ni tarehe 25 OKTOBA 2012.ADA YA KUJIANDIKISHA : Ada ya Kujiandikisha katika mradi huu ni Shilingi ELFU TANO tu ( Tshs. 5,000/= ) za Tanzania.
Ili Kujiandikisha, fika katika ofisi zetu zilizopo katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU.
MAHALI ZILIPO OFISI ZETU :
Kufika katika ofisi zetu, panda gari za UBUNGO- CHANGANYIKENI, kisha Shuka kituo kinaitwa TAKWIMU. Ukifika kituo cha TAKWIMU tembea hatua Ishirini kufuata barabara ya lami halafu upande wako wa kulia utaona bango limeandikwa RafikiElimu FOUNDATION.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa SIMU : 0763976548 AU 0782405936.EWE KIJANA WA KITANZANIA, TUMIA FURSA HII KUPATA UJUZI, UWEZO NA MAARIFA YATAKAYO KUWEZESHA KUTENGENEZA FURSA ZA KUJIAJIRI MWENYEWE