Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam jinsi vyakula vya asili vinavyoweza kuwavutia watalii kwenda kutembelea nchi mbalimbali na hivyo kukuza utalii wa nchi husika huku Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akimsikilia kwa makini. Mpishi Kapoor amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.
Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki leo jijini Dar es Salaam kitabu kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India. Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.