Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe.Said Suleiman Said ambaye pia ni Mbunge wa Mtambwe, akipokelewa na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Idara ya Magereza wakati yeye na wajumbe wenzake walipotembelea Gereza Kuu la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nchi wakati walipotembelea Gereza Kuu la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishiriki katika Kikao cha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI waliotembelea Gereza Kuu la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Mhe. Hamood Jumaa, ambaye pia ni Mbunge wa Kibaha Vijijini akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima wakati Kamati hiyo ilipotembelea maeneo mbalimbali ya Gereza Kuu la Ukonga, jijini Dar es Salaam.