Thursday, October 04, 2012

Mkuu wa Mkoa wa Mororgoro atembelea Msitu wa hifadhi ya asili wa Kumbulu



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bandera , Oktoba mosi  mwaka huu alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili katika Wilaya mpya ya Gairo. 

 Katika ziara hiyo, iliyomchukua kufika hadi Kata ya Chanjale, ambapo moja ya mambo ambayo aliyashuhudia ni suala la uharibifu mkubwa wa maliasili ya misitu kunakofanywa na baadhi ya watanzania wenye tamaa ya kuhitaji fedha za haraka. 

Hata hivyo Msitu wa hifadhi ya asili wa Kumbulu ,umeharibiwa vibaya kutokana na ukataji wa miti ovyo , uchomaji wa mkaa na upasuaji wa mbao , vitendo hivyo vikomeshwe mara m oja.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera pamoja na ujumbe wake wakiangalia lundo la Magogo yaliyokuwa yamekusanywa sehemu moja kwa ajili ya kuchomwa moto.
Askari Polisi wa Wilaya ya Gairo akifanya kazi ya kuharibu tanuli lililokuwa likichoma mkaa.
Msitu wa Hifadhi ya Asili wa Kumbulu ukiwa katika hatari ya kutokomezwa.
Wananchi wa kijiji cha Namba 30,kijiji cha Kumbulu wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera (hayupo pichani) juu ya hali ya uharibufu wa Mazingira.