Tuesday, October 16, 2012

MKUTANO WA TATHMINI YA SEKTA YA UVUVI, MISITU, WANYAMAPORI, MIFUGO NA UVUVI WAFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Washiriki wa mkutano wa tathmini ya maendeleo   ya sekta ya  Uvuvi, Wanyamapori, Misitu na Mifugo wakijadili masuala mbalimbali kuhusu usimamizi  endelevu wa maliasili  zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yahana Budeba akifungua mkutano wa wadau kutathmini maendeleo ya  ya Uvuvi, Wanyamapori, Misitu na Mifugo leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo uliowahusisha pia wadau kutoka nchi wafadhiri wa miradi ya maendeleo na wadau kutoka asasi za kiraia unalenga kuimarisha usimamizi wa maliasili na kupeleka madaraka ya usimamizi ngazi za vijiji.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yahana Budeba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya sekta ya Uvuvi, Misitu na Wanyamapori na hatua ya serikali ya kupeleka madaraka ya usimamizi  wa maliasili katika ngazi ya kijiji.
Washiriki wa mkutano wa tathmini ya maendeleo   ya sekta ya  Uvuvi, Wanyamapori, Misitu na Mifugo wakijadili masuala mbalimbali kuhusu usimamizi  endelevu wa maliasili  zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini leo jijini Dar es salaam.Picha Aron Msigwa-MAELEZO