Tuesday, October 16, 2012

Kutoka Tume ya Katiba:Mkoa wa Kaskazini Unguja watoa maoni yao juu ya Katiba mpya


 Wananchi wa Kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar wakifuatilia kwa makini mkutano ulioitishwa jana tarehe 13. Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo wenye malengo ya kukusanya maoni yao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba
 Bw. Said Haji Makame (21), mkazi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa jana tarehe 13. Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.
 Bi. Tatu Maalim Mganga (65) mkazi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa jana tarehe 13 Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.
 Bw. Yusuph Juma (60) mkazi wa Kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa jana tarehe 13. Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa mkutano ulioitishwa jana tarehe 13 Oktoba, 2012 na Tume hiyo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo. Wengine pichani (kutoka kulia) ni Wajumbe wa Tume hiyo, Joseph Butiku (kulia), Profesa Paramagamba Kabudi, Katibu wa Tume, Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki