Thursday, October 11, 2012

MGOGOORO WA VIBARUA NA MKANDARASI WAKWAMISHA SOKO MWANJELWA




MGOGORO uliozuka kati ya mkandarasi wa soko la Mwanjelwa linaloendelea kujengwa na vibarua huenda ukaathiri muda muafaka wa kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo baada ya shughuli za ujenzi kusimama.

Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Juma Idd, amesema kumekuwepo kutoelewana kati ya mafundi/vibarua na mkandarasi kutokana na kuchelewesha malipo.
  
Amesema kwa mujibu wa malalamiko ya vibarua pamoja na mafundi dhidi ya mkandarasi huyo ni kuwa fedha zimecheleweshwa; fedha zinazokadiriwa kuwa ni sh milioni 26 na hivyo kusababisha shughuli za ujenzi wa soko hilo kusimama kwa zaidi ya siku nne sasa.
  
Taarifa za mgomo huo zilifika ofisi za Serikali ya Jiji la Mbeya na kulazimika kufika katika eneo la soko na kuonana na mafundi hao.
  
Mkandarasi ametuma sh milioni 10 kwa ajili ya kupunguza deni kwa vibarua na mafundi na kwamba fedha zilizosalia bado wanafanya mawsiliano na mkandarasi.
  
Zoezi la kukabidhiwa soko lilikuwa lifanyike Oktoba 30 mwaka huu lakini kutokana na hali ya mgogoro huo na mambo mengine ya siri zilizopo zoezi hilo halitafanyika.
  
Imeelezwa kuwa soko hilo limekamilika kwa asilimia 75; vitu ambavyo bado ni upakaji wa rangi wa baadhi ya sehemu za soko na kuweka vioo katika baadhi ya sehemu za soko.

Vibarua wanaofanya kazi katika soko hilo ni 129 na mafundi 29 ndiyo walio na mgogroro na mkandarasi ambapo baadhi yao baada ya kutoridhishwa na ujenzi wa soko hilo waliamua kuacha kazi na kutoboa siri nzito za ubovu wa soko hilo Serikalini lakini wakapuuzwa na kuambiwa kuwa hawana akili timamu

kwa hisani ya kalulunga