Monday, October 08, 2012

MASHINE YA KUSAGA NA KUKOBOA YA KWAYA YA AIC BUZURUGA YAZINDULIWA RASMI LEO NA ASKOFU DANIEL NUNGWANA WA JIMBO LA MWANZA.



 Askofu wa AIC Jimbo la Mwanza Daniel Daud Nungwana ambaye ndiye mgeni rasmi ya hafla ya ufunguzi wa Jengo la Mashine ya Kusaga ya Buzuruga Super Sembe akishikilia mkasi ili aweze kukata utepe kulifungua huku wageni wengine waalikwa wakiangalia kwa umakini.
 Askofu Nungwana akimwomba Mungu ili aweze kuhusika katika shughuli nzima katika Mashine hiyo ya Buzuruga Super Sembe ya Kwaya ya Aic Buzuruga kutoka Mwanza.
 Kibao cha jiwe la Msingi ambacho leo kimewekwa wakafu na Askofu Nungwana katika ufunguzi wa Jengo la Kisasa la Mashine ya Kusaga unga wa Sembe.
                                                Mwonekano wa kibao kinavyosomeka...
                                                           Mtambo wa Kusaga..
Viongozi wa Kwaya ya Aic Buzuruga wamiliki halali ya jengo la Mashine ya Kusaga ambayo imezinduliwa leo na Mhashamu Askofu Daniel Nungwana.
Hii ni baadhi ya mitambo ambayo leo imeanza kazi kamili ya Kusaga unga safi wa Sembe ujulikanao kama Buzuruga Super Sembe.

                                           Ujazo wa unga kama unavyoonekana pichani.
                               Askofu Nungwana akisaini katika kitabu cha wageni.
                                                                   Meza ya Wageni...
 Mheshimiwa Mzee wa Trekta Mzee wa Kilimo Kwanza Lazaro Ng'weleja akifuatilia kwa makini shughuli nzima ya ufunguzi.
                                                            Joseph George Pamba..
 Mwenyekiti mstaafu wa kwaya ya Aic Buzuruga Shadrack Boaz na Mwenyekiti wa sasa kwaya ya Aic Buzuruga Antony David Ikongo wakisoma risala kwa Mgeni rasmi.
                                                         Aic Buzuruga wakiimba.
                                          Upande wa wale wa Mavocal kutoka Buzuruga.
                      Calvary Menonite Kwaya kutoka Bunda wakiimba katika hafla hiyo.
                        Ufunuo Kwaya kutoka PAG Makongoro wakiimbaa stejini.
                                                        Aic Muungano Kwaya...
 Huu ndiyo utumishi ambao wana wa Muungano Aic wanatumika. Hiii ni moja kati ya staili yaoooo. Utaipendaaaa ile mbayaaaaa.

                                                       Wageni waalikwaaa.
                                               Wageni watoto nao walikuwepo.

Waimbaji wa nyimbo za Injili wameombwa kutumia pesa kidogo wanazozipata kutokana na mapato ya kanda na mikanda yao ili kuanzisha miradi ya kuwaletea maendeleo katika utumishi wao.

Haya yamesemwa na Askofu wa Aic Jimbo la Mwanza Daniel Daudi Nungwana amabye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa jengo la mashine ya kusaga unga iitwayo Buzuruga Super Sembe ambayo ina uwezo ya kusaga na kukoboa tani moja na nusu kwa saa moja.

Askofu Nungwana amesema kuwa hii ni hatua njema sana katika kundi la Aic Buzuruga na kuomba waendelee kusonga mbele na kujizatiti zaidi ili kuhakikisha wanafikia malengo waliojiwekea.

Ametoa changamoto kwa vikundi vingine vya kwaya kuiga mfano wa kwaya hiyo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ili kuweza kurahisisha kazi ya utumishi katika shamba la Mungu.

Jumla ya shilingi milioni tano laki tisa elfu themanini na nane na mia tano zimeapatikana kutokana na Michango ambayo wageni waalikwa na wahisani mbalimbali wametoa kwa ajili ya kuwaspaoti waendelee mbele katika kuifanya kazi yao vizuri.

Aidha mwenyekiti wa kwaya ya Aic Buzuruga Antony David Ikongo ametoa shukrani kwa niaba ya kwaya ya Buzuruga kwa wageni na watu waote waliojitokeza kuwasapoti kwenye ufunguzi wa mradi wao wa Buzuruga Super Sembe.