Monday, October 08, 2012

Mapokezi ya Timu ya Elimu Sports Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi



Timu ya Elimu Sports Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imepokelewa leo na Kaimu Katibu Mkuu Bw. Salum Mnjagila,viongozi wengine wa wizara na wafanyakazi baada ya kuwika katika mashindano ya SHIMIWI mwaka huu yaliyomalizika Jumamosi mjini Morogoro. Timu ya soka ya Elimu Sports imetawazwa mabingwa baada ya kuichapa National Audit, aidha, timu ya Riadha ya wizara imekuwa mshindi wa jumla wa mchezo huo na imenyakua ushindi wa pili katika mchezo wa Darts.
Kaimu Katibu Mkuu Bw. Salum Mnjagila akipokea kombe la ubingwa wa mpira wa miguu katika mashindano ya SHIMIWI mwaka huu
Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakifurahia vikombe vya ushindi walivyovipata
Picha ya pamoja ya viongozi wa wizara na wanamichezo wa Elimu Sports. Picha na habari na ntambi bunyazu