Friday, October 05, 2012

Mahusiano ya Tanzania na India kuzidi kuimarika - Spika Makinda




Spika wa Bunge la India Mhe. Meira Kumar akimkaribisha mgeni wake, Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Anne Makinda kwenye chumba maalum kwa ajili ya mazunguzo kuhusu ushirikiano wa nchi mbili hizi .
Mhe. Makinda akisaini kitabu cha wageni mashuhuri huku akiongozwa na mwenyeji wake, Mhe. Kumar.
Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo ya kina kuhusu mahusiano ya Tanzania na India, wakati ujumbe huo ukimsikiliza Spika wa Bunge la India.
Pokea zawadi kutoka Tanzania… ndivyo Spika Makinda anavyomwambia mwenyeji wake.
Baada ya mkutano wa Saba wa Maspika wa Bunge wanawake kumalizika, viongozi hao kwa pamoja walikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza yaliyojiri.
Kwaheri na karibu Tanzania
Ujumbe wa Tanzania na ule wa india katika picha ya pamoja. Picha na Prosper Minja-Bunge