Washiriki wa mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) ambayo ni maalum kwa mikoa ya kanda ya ziwa wakiendelea kupiga makasia wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika Wilayani Bukoba Mkoani Kagera hivi karibuni,ambapo zaaidi ya timu 50 zenye watu watano kila timu zilishiriki na walishindana kupiga kasia kwa umbali wa Kilometa 3 kwenda na kurudi
Michuano ya nguvu ikiendelea Majini ndani ya Ziwa Victoria.
Meneja wa Bia ya Balimi Edith Bebwa(kulia) akizungumza na washiriki wa mashindano ya Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani Kagera mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo timu tano zitakwenda kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali zitakazofanyika mkoani Mwanza Disemba mwaka huu.
Katibu tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiamukama, akifungua mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika Wilayani Bukoba Mkoani Kagera ambapo zaaidi ya timu 50 zenye watu watano kila timu zilishiriki, ambapo walishindana kupiga kasia kwa umbali wa Kilometa 3 kwenda na kurudi, kushoto ni Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Ziwa Endrew Mbwambo na Afisa wa Sumatra Kapteni Alex Katama.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoani Kagera upande wa wanaume timu ya Kabanga Bushasha wanaume wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki tisa (900,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiomukama, akimkabidhi kitita cha Tsh.900,000 Nahodha wa timu ya Kabanga Bushasha, Eliudi Prospa baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya (Mitumbwi) Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani Kagera jana ambapo washiriki walishindana kuendesha mitumbwi kwa makasia.