Saturday, October 13, 2012

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Auwawa.



                                             LIBERATUS BARLOW ENZI ZA UHAI WAKE
KAMANDA WA POLICE MKOA WA MWANZA BWANA LIBERATUS BARLOW AMEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WANAO HISIWA KUWA NI MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO. MAREHEMU ALIUWAWA NJIANI MAJIRA YA SAA TISA USIKU AKIELEKEA NYUMBANI KWAKE AKITOKEA KWENYE KIKAO CHA HARUSI.

KUUWAWA KWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ,IGP MWEMA ATUMA KIKOSI MWANZA.
Mkuu  wa  jeshi la  polisi (IGP) Said Mwema amethibitisha  kuuwawa kwa kakamnda  wa  Mwanza Liberatus Barlow .Amesema  kuwa  kamanda  huyo wa polisi ameuwawa na  watu  wanaosadikika kuwa ni majambazi majira ya saa 7.30  na saa 8 usiku   katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.Mwema amesema  kuwa kamanda  Barlow alikuwa akitokea katika  kikao cha harusi akiwa njiani kumrudisha dadake nyumbani kwake ghafla  alikutwa na tukio  hilo la  kupigwa  risasi.

Hata  hivyo alisema  kuwa  kutokana na tukio  hilo jeshi la  polisi  linataraji kuanza uchunguzi  wake kuanzia leo na timu ya askari  kutoka  makao makuu ya polisi  wataondoka mapema leo kwenda  jijini Mwanza  kuungana na askari wa mkoa  huo kwa ajili ya uchunguzi  zaidi na msako wa majambazi hayo .Mwema amewataka  wananchi  wa Mwanza  kutoa ushirikiano wao kwa  jeshi la polisi ili kufanikisha  zoezi hilo na  kuwataka kutokuwa na hofu  yoyote kutokana na tukio  hilo.