Friday, October 19, 2012

BREAKING NYUZZZZ: WAISLAM JIJINI DAR WAANZA MAANDAMANO MCHANA HUU,VURUGU KUBWA LAZUKA KARIAKOO

-->
Ikiwa leo ni siku ya pili tangu vurugu zilizoanza jana zinazofanywa na Waumini wa dini ya Kiislam kutetea maslahi ya Waislam kutoka kwenye mfumo dume uliopo Tanzania.

Siku Ya Jana Maandamano yalikuwa rasmi kwa ajili ya Kupinga kukamatwa kwa Katibu Wa Wanaharakati wa Kiislam Shekhe Ponda Issa Ponda ambapo walikuwa wakishinikiza Kuachiliwa kwa shekhe huyo aliyefikishwa Mahakami siku ya Jana. Leo Waumini hao walishinikiza Serikali kama Mpaka Mchana swala ya Ijumaa itakapokuwa inamalizika kama shekhe huyo hata achiliwa basi wataandamana Jiji zima kushinikiza kuachiliwa kwa shekhe huyo.

Mchana wa leo majira ya saa 6 Mkuu wa Mkoa wa Dar, aliutangazia uma kupitia Radio One kuwa Maandamano hayo hayana baraka za Serikali ni Batili, hivyo watu wasiandamane. Mara baada ya swala ya Ijumaa Waislam wakakaidi amri hiyo kwa kuandamana.

Hii ni wiki ya nne Waislam kuandama kila baada ya Swala ya Ijumaa, wiki iliyopita Waumini wa dini hiyo walichoma Makanisa Kadha wa Kadha kuonesha hasira zao za Kijana mwenye umri wa miaka 12 kukojolea kitabu chao Kitakatifu cha Quran.

Leo Jeshi la Polisi, FFU na Jeshi la JWTZ wamefanikiwa kutawanya maandamano hayo yaliyotokea kona mbali mbali za Dar, maeneo ambayo mabumu ya machozi yalitumika ni Kariakoo, Posta Mpya, Magomeni, Kinondoni na Maeneo ya Buguruni.
 Muumini Wa Dini Ya Kiislam aliyekamatwa siku Ya Jana
 Wanajeshi wa JWTZ wakijiweka Sawa Siku Ya Leo Maeneo Ya Morocco
 Kikazi Zaidi
 Posta Mpya inavyoonekana Saa Chache zilizopita
 Hii Ilikuwa Mbagala Wiki Iliyopita
 Wazee wa TIGO, wakiwa Ndani ya Clock Tower Dar-es-Salaam leo Mchana
 Wazee Wa Kazi Wakiwa wamejipanga
Kariakoo.