Wednesday, September 19, 2012

ZAIDI YA WATAHINIWA LAKI 8 LEO WANAFANYA MTIHANI WA KUMALIZA DARASA LA SABA. YAPI MATARAJIO YETU?



 
 Jumla ya watahiniwa 894,881 leo wanafanya mtihani wao wa kumaliza elimu ya msingi wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri na kuvuka salama kipimo hicho ambacho kitatoa tathmini ya kile ambacho wamekuwa wakikifanya kwa kipindi cha miaka saba.  
Natumaini kwa mfumo mpya utakaotumika, makosa madogo madogo yaliyokuwa yakijitokeza ama kwa bahati mbaya ama kwa baadhi ya watu kukusudia hayatajitokeza.
Ni miaka takriban 50 sasa tumekuwa tukizalisha wanafunzi wa sekondari kwa mfumo wa mtihani wa darasa la saba, lakini ipo tofauti kubwa sana kati ya ufaulu wa zamani na wa sasa.
Je Tatizo ni mfumo wa elimu, uwezo wa waalimu, mtaala wa masomo, sapoti ya serikali au wanafunzi wenyewe?
Tunawatakia ufaulu mwema wa kweli wa kiwango cha juu huku kiwango cha udanganyifu kikishuka kwa kasi.