Sunday, September 16, 2012

Yusuf Kalala na mke wake Sharifa Kalala wadai kuitapeli kampuni ya Mokha Agency Co. Ltd kwa kutumia jina laaliyekua Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.



Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Wakala wa kupakia na kupakua mizigo bandarini ya Mokha Agency Co. Ltd, Mohamed Lema akionesha Taarifa ya Polisi (RB) kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo waliyofungua katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi baada ya watu waliofahamika kwa majina ya Yusuf Kalala na mke wake Sharifa Kalala kuitapeli kampuni hiyo kiasi cha fedha shilingi milioni 11.1 kwa kujipatia huduma kwa njia ya udanganyifu wakutumia jina la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Katikati ni Msemaji wa kampuni hiyo, Salim Dawa na mmoja wa wanafamilia hiyo, Amin Kulateni.