Wakati wa kusifu na kuabudu katika kanisa la EAGT City Centre kama inavyoonekana katika picha ambapo kamera yetu ililinasa tukio hili katika ibada ya jumapili ya leo. Wapiga vyombo wa Kanisa la City Centre wakionekana wakiwa wanafanya kazi yao kama kawaida.
Wakati wa kumsifu Mungu hakuna ambaye anaambiwa cheza hivi au fanya hivi, hapa kila mmoja anamchezea Mungu kwa jinsi Mungu alivyotenda Mambo makuuu katika maisha yake.
Praise team kutoka kanisa la City Centre wakiimba kwa umakini sana kwa sauti nzuri ambazo Mungu amewapa.
Hawa ni wakristo ambao wameleta Fungu la Kumi, moja kati ya hatua ya mkristo katika makuzi ya kiroho. Kama wewe ni mkristo ni wajibu wako kutoa fungu la kumi kwa yote unayopata katika biashara yako.
Kwaya ya EAGT City Centre wakiimba wimbo mzuri sana ambapo kila mkristo aliyefika katika kanisa hilo alibarikiwa, hapa soloist Mr Paulo anaongoza kikosi kazi cha kwaya hiyo.
Kwa Yesu kuna raha sanaaaaa.
Wanacheza kwa staili nzuri kama inavyoonekana.
Wakristo wa kanisa hilo wakisikiliza neno la Mungu kwa umakini huku wakiendelea kupokea upako wa Mungu ambao si wa kawaida.
Kwa Mungu mambo kama haya yapooo, wala usihofu.
Wakristo wakionekana wamejaa upako sana na huu ni upande wa kina baba kama walivyokamatwa na kamera yetu katika ibada ya Jumapili.
.Wakristo wakumbushwa jinsi Mungu alivyo mkuu.
.Waambiwa wasisumbukie maisha.
Wakristo wamekumbwa kuwa na Yesu siku zote katika maisha yao na kuendelea mbele na safari ya kwenda mbinguni kwa kuwa wanakabiliwa na mambo magumu sana katika maisha ya kila siku na hivyo kama hawatakuwa makini wanaweza wasimalize safari yao vizuri.
Haya yamesemwa na Mtumishi wa Mungu Mama Mchungaji Amasi katika ibada ya jumapili katika kanisa la EAGT City Centre kanisa linalioongozwa na Mchungaji Michael Kulola wakati akihubiri neno la Mungu katika kusanyiko la Watu wa Mungu.
Amesema kuwa maisha ni muunganiko wa mambi mengi sana na yote yanamkabili mkristo na kuomba kuwa makini katika kuyakabili yote yanayokuja mbele yake na kumwomba Mungu sana kila mara ili aweze kukupa ngvu katika kushinda majaribu yote amabyo shetani anayaleta katika maisha ya kila siku katika mkristo.
Ametoa mfano kuwa watu wengi wamepoteza mwelekeo wa Mungu na kushindwa kuendelea katika safari ya kwenda mbinguni kwa kuweka mbele suala la maisha mbele hivyo kupoteza kila upako wa thamani ambao mkristo ameupata wakati alipokubali kuokoka na kuwa mfuasi wa Yesu kristo.