Sunday, September 30, 2012

TRENI YA TAZARA ITAKAYOTUMIKA KWA USAFIRI WA DAR ES SALAAM –MWAKANGA-KURASINI YAFANYIWA MAJARIBIO



 Treni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),likiwa katika stesheni ya Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya Majaribio iliyofanyika kutoka Dar es Salaam-Mwakanga-Kurasini-Dar jna mchana. Treni hiyo kwa kuelekea Mwakanga itapita  Kwa fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo(Kigilagila), Sigara, Kitunda, Kupunguni B, Majohe, Magnus na Mwakanga. Na kuelekea Kurasini Itatokea Dar,Kwa fundi Umeme,Yombo,Chimwaga,Maputo,Mtoni Relini,Kwa Azizi Relini na kishia Stesheni ya Kurasini.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA)na wa Wizara ya Uchukuzi wakiwa ndani ya Mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio kwa ajili ya Usafiri wa treni Jijini Dar es Salaam jana.

 Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),Mhandisi Abdalla Shekimweri akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo jana wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yakayofanya safari zake kutokea Dar-Kurasini-Mwakanga.Mabehewa hayo ni sehemu tu ya mabehewa yatakayokuwa yakifanya safari hizo.

Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), Mhandisi Abdalla Shekimweri,akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (aliyevaa shati la rangi ya zambarau)katika kituo cha Mwakanga wakati wa majaribio ya mabehewa matatu ya TAZARA yatakayotumika kwa Usafiri wa Dar es Salaam jana.Mabehewa hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 80 waliokaa kwenye Siti na yanatarajiwa kuanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam-Mwakanga na Dar es Salaam-Kurasini kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu.