Tuesday, September 18, 2012

SCF yawapa wajasiriamali mbinu za kibiashara



 
Mkurugenzi wa Mfuko wa Kukuza ushindani kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SCF) Casmir Makoye akifafanua jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya kipekee ya awamu ya tatu kwa wajasiriamali wadogo na wakati usindikaji wa chakula, inayofanyika mjini Morogo, kwa lengo la kujenga uwezo wao wa ndani ya kuzalisha bidhaa bora na kuongeza faida. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Kilimo na Biashara ya Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo- (SUA - DAEA) Dr Damas Philips na kulia ni mratibu wa mafunzo hayo na mhadhiri kutoka SUA Akyoo Meshack.
 
Mkurugenzi wa Mfuko wa Kukuza ushindani kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SCF) Casmir Makoye (kulia) alifurahia jambo na Mkuu wa Idara ya Uchumi Kilimo na Biashara ya Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo- (SUA - DAEA) Dr Damas Philips muda mfupi baada ya kufungua rasmi mafunzo ya kipekee ya awamu ya tatu kwa wajasiriamali wadogo na wakati usindikaji wa chakula, inayofanyika mjini Morogoro.
 
Mkurugenzi wa Mfuko wa Kukuza ushindani kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SCF) Casmir Makoye (kulia) alifurahia jambo na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo-Idara ya Uchumi Kilimo na Biashara ya Kilimo (SUA - DAEA) Dr Damas Philips (wapili kulia), Dk Zena Mpenda (watatu kulia) na Felix Nandonde, ambao ndo wawezeshaji wa mafunzo ya aina yake kwa wajasiliamali usindikaji wa chakula iliyoandaliwa na SCF na kufanyika mjini Morogoro.

======  ========  =======

SCF yawapa wajasiriamali mbinu za kibiashara

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Mfuko wa kukuza ushindani kwa wajasiriamali wadogo na wakati (SCF) inaongeza kasi ya kutoa mafunzo yakipekee kwa wajasiriamali wadogo na wakati wanaosindika bidhaa vya vyakula nchini ili kujenga uwezo wao wa uzalishaji wa bidhaa bora na kuongeza faida yao.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo jana ya awamu ya tatu yatakayo chukua wiki moja mjini Morogoro, inayowahusisha Wakurugenzi Watendaji na wafanyakazi wa makampuni yanayosindika vyakula  nchini, Mkurugenzi wa SCF, Bw. Casmir Makoye alisema kuwa taasisi yake inatazamia kuwasaidia wajasiriamali kujenga uwezo wao wa kuzalisha bidhaa bora ambayo yatakidhi vigezo vya ushindani ndani na nje ya nchi, pamoja na mbinu za upatikanaji wa masoko hususani katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Bw. Makoye alisema kuwa dhamira kubwa ya mafunzo hayo ni kuwapatia elimu na ujuzi wasindikaji wadogo na wakati ambayo yatawapatia uwezo wa kuzalisha bidhaa zitakazokidhi vigezo vya kimasoko na bidhaa ambazo zitakuwa zimefikia ubora inayokubalika katika soko la ndani na la kimataifa.

“Zaidi ya wajasiliamali 100 katika nyanja ya usindikaji wa chakula wanatarajia kufaidika na mafunzo haya yakipeke ambayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kushindana kibiashara katika soko la ndani na la kimataifa,” alisema.

Aidha Bw. Makoye alisema kuwa taasisi yake imepanga kufanya mafunzo mengine mwezi Oktoba mwaka huu, ambayo itajikita katika usindikaji wa maziwa ambapo wafanyabiashara wadogo na wakati watafundishwa jinsi ya kuzalisha bidhaa za ziada mbali na kuendelea a uzalishaji uliozoeleka ya kuzalisha jibini, mtindi na siagi. Pia watapata fursa yakufundishwa jinsi ya kuongeza vionjo zaidi katika bidhaa zao.

Mafunzo yanayoendeshwa na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine -Idara ya Kilimo cha Uchumi na Biashara ya Kilimo (SUA - DAEA) chini ya mwamvuli wa (Chuo Kikuu cha Sokoine Kilimo - Tume ya Ushauri wa Kilimo (SUA BACAS), kinatarajia kuwapatia washiriki elimu ya uongozi katika biashara itakayowasaidia kufanyabiashara zao kiushindani kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora katika gharama nafuu na kuwa na njia nzuri za utafutaji wa masoko.

Mkuu wa Idara ya Uchumi Kilimo na Biashara (SUA - DAEA) Dk Damas Philips alisema kuwa mafunzo yatasaidia wafanyabiashara wadogo na wakati kuongeza uwezo katika uongozi ndani ya kampuni zao, kuboresha njia za usambazaji wa bidhaa zao na kuwapatia njia bora za jinsi ya kuhifadhi  vyakula kwa kufuata viwango vya ndani na vya kimataifa.

Dkt Philips alisema kuwa katika utafiti uliofanywa na SCF, mapungufu yaliyojitokeza ni pamoja na utambuaji wa fursa zinazojitokeza za masoko, pale ambapo wafanyabiashara wadogo na wakati wanaweza kuuza bidhaa zao, lakini idadi ya bidhaa zao ni ndogo na bei zao si za kiushindani kutokana na gharama za uzalishaji kuwa juu.

"Upatikanaji wa njia sahihi ya utafutaji masoko, ambapo SMEs nyingi zinapoteza uelekeo na kutumia rasilimali zao vibaya, na hivyo kupoteza wateja wa bidhaa zao.

"SMEs nyingi nchini zinakuwa na mipango isiyo rasmi katika kuwezesha kufikisha bidhaa zao sokoni, hawana njia nzuri za kuandaa mipango thabiti ya utafutaji masoko ili kufikia malengo yao. Wengi wanadhani ni gharama kutengeneza mikakati na kuiweka kisasa pamoja na kuhusisha wataalam kuwasaidia kutengeneza mpango ya kibiashara uliyothabiti, "alisema Dk Philips.

Mapema mwaka huu SCF ilianzisha Mfumo wa upatikanaji wa taarifa za vituo ya masoko (POS database) ambao sasa unapatikana kwa matumizi ya wasindikaji wa vyakula nchini kwa gharama ya dola za Marekani 100, mfumo ambao itawasaidia kupata kwa urahisi taarifa muhimu za soko utakaowasaidia kupanua wigo wao wa mauzo na kuongeza mauzo ya bidhaa zao kwa ujumla.