Monday, September 24, 2012

MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE APATIKANA NI EUGENE FABIAN



Miss Eugene Fabian (katikati)kutokea mkoa wa Mara ndiye mshindi wa shindano la Redd,s Miss Lake Zone 2012,Lililofanyika usiku wa jana  mjini kahama na kuwashirikisha warembo kutoka mikoa 6 ya kanda ya ziwa.

  Redd's Miss Lake Zone 2012, Miss Eugene Fabian katika picha ya pamoja na mshindi wa pili na watatu katika shindano hilo ambalo warembo wa mkoa wa Kagera hawakuweza kutamba kabisa,ambapo nafasi ya tatu imechukuliwa na Miss Happiness Rweyemamu kutoka  mkoa wa Shinyanga (pichani kushoto)na mshindi wa pili ni Miss Happiness Daniel(kulia) kutoka Mwanza. Washindi hawa watatu watawakilisha Kanda ya ziwa katika shindano la taifa linalotarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao. Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni  kitita cha shilingi Laki 7, mshindi wa pili laki 5 na mshindi wa tatu laki nne na nusu !!!