Tuesday, September 25, 2012

MKUU WA MKOA WA MWANZA ENG. EVEREST NDIKILLO AFUNGUA MAADHIMISHO YA 33 YA UTALII DUNIANI AMBAYO KITAIFA YANAFANYIKA JIJINI MWANZA.



 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Everest Ndikillo katikati akiwa na mwenyekiti wa Mwanza Tuorism Association John Rubambe kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Henry Mabiti wakiangalia wachezaji wa ngoma za jadi uwanja wa Nyamagana leo kwenye ufunguzi wa Wiki ya Utalii duniani ambayo kitaifa inafanyika Mwanza.
Esther Morris wa Mwanza Review Magazine na akiangalia kwa umakini mazuri yote yanayoendelea uwanjani hapo.
 Viongozi mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia shughuli nzima ya ufunguzi wa wiki ya Utalii duniani jijini Mwanza.
 Chifu Ilago Kamphipa aliye Mwenyekiti wa Machifu wa Mkoa wa Shinyanga na Mwanza akisaliamiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Henry Mabiti huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Everest Ndikillo akifanya utambulisho wa wageni waliokuwa katika msafara wake.
 Chifu Itale Dotto wa Bujashi Shinyanga na Chifu Ilago Kaphipa wakiwa wamekaa wakitazama mazuei yote yanayoendelea uwanjani hapo leo.
 Chifu Ilago Kaphipa akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza moja kati ya kifimbo cha kitamaduni kama inavyoonekana pichani.
                                                             Wageni Waalikwaaaa.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Everest ndikillo ambaye ndiye Mgeni rasmi wa ufunguzi wa wiki ya Utalii duniani akitembelea mabanda mbalimbali uwanjani hapo leo.
                                                   Banda la Bujora lenye mapishi asilia.
                                                 Banda la kampuni ya simu ya Tigo...
                                                                       Chui

                                                                          Fisi
                                                                         Ndege.
                                                                         Mzee Kobe.
                                                Banda la Wizara ya Mali asili na Utalii..
                                                                Majiko ya asili.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akiserebuka baada ya kupambwa na Mzuka wa Ngoma ya Mang'ombe za kijiji kutoka Wilaya ya Misungwi.
 Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mama Lugaila nae akishindwa kuhimili vishindo vya ngoma akaamka kucheza.

                                               Ngoma aina mbalimbali uwanjani hapo..

WATANZANIA wametakiwa kutangaza vivutio vya Utalii ili kuweza kuinua kipato na uchumi wa Nchi ya Tanzania.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Everest Ndikillo katika ufunguzi wa wiki wa Utalii duniani ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Mwanza.
Akijibu risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Mwanza Tourism Association John Rubambe amesema kuwa Tanzania inayo vivutio vingi na kinachotakiwa ni kuzitangaza ili watalii waweze kuvijua na kuja kuviona.

Amevitaja baadhi ya vivutio hivyo kama vile Ziwa Victoria, Ngoma za jadi za kisukuma ambazo hiko Bujora Jijini Mwanzam Jiwe linalocheza lililoko Wilayani Ukerewe na vingine vingi.

Amesema utalii unachangia pato na kuinua uchumiwa Tanzania  kwa fedha za kigeni    na kusema kuwa ili watalii waendelee kuja Tanzania kwa wingi lazima kuvitangaza vivutio hivi ambayo zinapatikana Tanzania.

Pia amesema watalii wamekuwa wakiongezeka kwa wingi kila mara na  kutoa wito wa taasisi ya fedha kama mabenki kutoa pesa kwa wajasiliamali wadogo wadogo ili kupanua biashara yao.

Aidha amesema ili Tanzania ipate matokeo chanya katika nyanja ya utalii ni lazima watanzania pamoja na serikali kuwa mstari wa mbele kutangaza utalii wa Tanzania na kutoa wito kwa Serikali kuuita Uwanja mkubwa utakaojengwa Mwanza kama Serengeti International Airport.

Haya ni Maadhimisho ya 33 Wiki ya utalii duniani ambayo  yameanza leo jijini Mwanza na kilele chake kitafanyika tarehe 27 septemba mwaka huu na kitaifa yanafanyika jijini Mwanza na.