Monday, September 17, 2012

Mbunge wa Jimbo la Kitope na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Agawa Taa zinazotumia mwanga wa jua jimboni kwake



 Muanzilishi wa Mradi wa Taa zinazotumia mwanga wa Jua wa Kampuni ya Wakawaka ya Nchini Uholanzi Bwana Maurits Groen akifahamisha namna ya matumizi sahihi ya Taa zinazotumia mwanga wa jua kwa Wananchi wa Kijiji cha Matetema na Kichungwani ndani ya Jimbo la Kitope ambao walibahatika kupata msaada huo.Kushoto yake ni Mbunge wa Jimbo la Kitope na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Kulia ni Mkurugenzi masoko wa Kampuni ya Wakawaka Bwan Bill Carney.
 Mbunge wa Jimbo la Kitope na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Vijiji vya Matetema na Kichungwani ndani ya Jimbo lake katika hafla  ya ugawaji wa Taa zinazotumia mwanga wa jua zilizotolewa msaada na Kampuni ya Wakawaka ya Nchini Uholanzi.Kulia yake ni Muanzilishi wa Mradi wa Taa hizo wa Kampuni ya Wakawaka Bwana Maurits Groenna kushoto yake ni Mkurugenzi Masoko wa Kampuni hiyo Bwana Bill Carey
 Mbunge wa  Jimbo la Kitope na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi mmoja miongoni mwa wananchi kadhaa wa  Vijiji vya Matetema na Kichungwani Taa inayotumia mwanga wa jua zilizotolewa msaada na Kampuni ya wakawaka ya nchiniUholanzi.
Muanzilishi wa  Mradi wa Taazinazotumia mwanga wa Jua kutoka Kampuni ya Wakawaka ya Nchini Uholanzi Bwanan Maurits Groen akimkabidhi Taa inayotumia mwanga wa jua mmoja wa wananchi kadhaa wa Vijiji vya Matetema na Kichungwani ndani ya Jimbo la Kitope.