Mratibu wa mpango wa ujenzi wa Shule ya Green City, Timothy Levy (kushoto), akimkabidhi cheti cha shukrani Shy-Rose Bhanji, kwa kuunga mkono jitihada za kufanikisha ujenzi wa shule hiyo ya watoto yatima.
Mbunge wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji (kulia), akikabidhi msaada ya Shillingi millioni 1 kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Hananasif Orphanage Centre, Hezekia Mwalugaja (kushoto), ambacho kinajenga shule ya Sekondari (kidato cha tano na sita ) Wilayani Rungwe, Mkoani Mbeya. Shule hiyo ya Green City, itakuwa ni kwa ajili ya kusomesha watoto yatima. Katikati ni Mratibu wa Mpango huo Timothy Levy. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam jana
Shy-Rose Bhanji ambaye pia ni Mwanaharakati wa masuala ya kijamii (katikati), akitoa wito kwa wadau mbalimbali kujitolea michango ya hali na mali kufanikisha ujenzi wa shule ya Watoto Yatima ya Green City, ambayo hivi sasa ujenzi wake umeshafikia kwenye hatua ya msingi kwa madarasa manne pamoja na Ofisi za Walimu.