Tuesday, September 25, 2012

Mama Kikwete ahudhuria mkutano wa wake wa viongozi wa Afrika jijini New York, Marekani



 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa majadiliano ya kubadilishana mawazo kuhusu  namna ya  kuwasaidia na kuwahamasisha  wanafunzi   kushirikia katika masomo ya  Sayansi, Tekinolojia, Uhandisi na  Hesabu Mkutano huo ambapo  uliandaliwa na Bi Savannah Maziya Mkurugenzi  Mtendaji wa Bunengi Gropu kwa kushirikiana na Makampuni mengine na kupewa jina la  la African First Ladies Roundtable, Umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la  Suisse America , jijini New York na kuhudhuriwa na  baadhi ya  wake wa marais,  wakurugenzi wa makampuni mbalimbali, wanadiplomasia na wahadhiri.

Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na   Bibi Katalin Bogyay Balozi wa  Hungary UNESCO na amebobea katika diplomasia ya utamaduni  na mtetezi mkubwa wa masuala yahusuyo  fursa sawa ya elimu kwa mtoto wa kike.