Saturday, September 22, 2012

Kanisa Katoliki Lapata Mashemasi


 Lango la kuingilia Jordan University College,tawi la St.Augustine University mali ya Kanisa Katoliki
 Kikanisa (chapel) kilichopo chuoni hapa
 Mhashamu Telesphor Mkude,Askofu Katoliki wa jimbo Katoliki la Morogoro wakati wa mahubiri kwenye misa ya kuweka mashemasi
 Akiketi kwa kwa ajili ya makandidati wa ushemasi kuahidi utii kwa maaskofu na wakuu wa mashirika yao
 Mashemasi watarajiwa mbela ya askofu

 Mmoja wao Frt.Elias Nyamironda wa shirika la Mt.Vincent wa Paulo akiahidi utii kwa askofu


 Mashemasi watarajiwa wakiwa wamelala kifudifudi (prostrate),ishara ya utii kamili kwa Mungu.wakati huu huimbwa litania ya watakatifu wote,kuwakabidhi watarajiwa katika maombezi ya kanisa zima.kisha litania askofu husali sala ya wakfu na ushemasi huwashukia.
 Baada ya sala ya wakfu sasa ni mashemasi.na hapa huvalishwa vazi la cheo chao (Dalmatic).hapa Mheshimiwa Shemasi Elias Nyamironda wa Shirika la Mt.Vincent wa Pauli akivalishwa kawaida na padre
mashemasi katika mavazi rasmi ya ushemasi

Ushemasi ni kati ya daraja tatu katika Kanisa Katoliki. Ushemasi(Diaconos),upadre (Presybyteroi) na uaskofu(Episcopoi).baada ya masomo ya falsafa miaka 3,na theolojia miaka 4,mtu hupata daraja hii,kisha baada ya miezi michache kama 6 hivi hupewa upadre.