Friday, September 21, 2012

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) yaipiga jeki BFT


Onesmo ngwi
--
Rais huyo aliyekuwa bondia maarufu wakati wa ngumi za ridhaa na kulipwa miaka ya 80 na 90 kiasi cha lupewa jina la "Piston Mover"(mwendo wa piston ya gari) kwa ajili ya kasi ya mikono na miguu yake alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufundisha ufundi kwa mabondia ili waweze kucheza ngumi za ufundi. 

"Kuna tofauti kubwa sana kati ya ngumi za ridhaa na ngumi za kulipwa" aliendelea kusisitiza Rais huyo.

"Wakati mabondia wa ridhaa wanapewa points wakati wanapopiga ngumi za ufundi za kichwani, bondia wa ngumi za kulipwa anatakiwa aweze kumzidi mpinzania wake kwa kila kitu" aliendelea kusisitiza Rais huyo.

Mabondia wetu wa ridhaa wanatakiwa wafundishwe namna ya kupiga ngumi za ufundi kichwani na ziwe nyingi ndipo wanaweza kushinda kwenye mashindano ya kimataifa" alimalizia kusisitiza Ngowi.

Ushirikiano wa TPBC na BFT unaleta sura mpya kwenye tasnia ya ngumi nchini na inaonyesha mwanga mzuri mbele ta safari.Mgeni rasmi katika fainali za mashindano hayo alikuwa ni Katibu Mkuu wa BMT bwana Henry Lihaya na alimshukuru Ngowi kwa msaada huo wa TPBC.

 Aidha, Ngowi alikabidhi baadhi ya zawadi kwa washindi walioshinda katika fainali hizi za mwaka 2012.