Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished Bade (pichani), kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Taarifa iliyotolewa Jumatano, Septemba 19, 2012 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais - Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo umeanza Jumatatu wiki hii, Septemba 17, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Bade alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Mortgage Finance Co. Ltd.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Septemba, 2012