Friday, September 14, 2012

FFU wakumbana na washabiki waliodata akili Mjini Bremerhaven,Ujeruamani



FFU wa Ngoma Africa band  watembeza gwaride la kufa mtu  Ughaibuni, Bremerhaven,Ujerumani,

Katika Jumba la ajabu palikua hapatoshi

Siwengine bali ni Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU,yenye maskani yake nchini Ujerumani
bendi hiyo maarufu siku ya jumatano 12.9.2012 ilijikuta ikivaana jino kwa jino tena na washabiki sugu
ndani ya juma la ajabu la "Klimahaus" Arena mjini Bremerhaven,Ujerumani.
Baada ya mdundo wa ngoma africa band kupenya katika nyoyo za washabiki wa mataifa mbali mbali 
walifurika katika onyesho hilo wengi wao wakiwa wenyeji wa ulaya.uwanja wa dansi ulionekana
mdogo na kukawa na patashika la nguo kuchanika.
Washabiki waliodata akili walijikuta wakiperekana samba samba na muziki wa ngoma africa band,
kiasi cha kuwafanya walinzi wa usalama kufanya kazi ya ziada kuhakikisha kila kitu kipo salama.
Ngoma Africa band aka ffu au maarufu kwa majina mengi ya utani kama vile "Watoto wa Mbwa"
"wazee wa bongo tambarare" kutoka katika kabila la "Wagagagigikoko" waliogunduliwa katika
Maadiko ya kitabu cha Buri Cheka watatumbuiza tena siku ya Jumamosi 15.09.2012 katika
Maonyesho ya AFRIKA-MESSE mijini Bremen,Ujerumani.
Usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com