Mwenyekiti wa serikali ya mtaa ya Manzese-Uzuri, Jonas Ismail, akiongea na mtandao huu katika ofisi hizo.
…Akionyesha fomu kwa ajili ya Watanzania katika zoezi hilo.
…Akitoa elimu kwa watu wenye kujiandikisha.
Wananchi wakijaza fomu za zoezi hilo.
Jonas Ismail akiongea na raia wa Malawi aliyetaka kupata kitambulisho cha muda.
…Akionyesha fomu wanazojaza raia wa nchi za nje.
Mmalawi aliyenaswa akiwa anasoma gazeti la Uwazi.
ZOEZI la kutolewa vitambulisho vya taifa limeendelea kwa matatizo
mbalimbali yanayotokana na uelewa na elimu ndogo iliyotolewa kwa
wananchi kuhusu zoezi hilo, hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na
mtandao huu katika jiji la Dar es Salaam ambako wananchi wengi
wameelezea kuwepo na mkanganyiko mkubwa kuhusiana na kile wanachotakiwa
kufanya ili kukamilisha jukumu hilo.Pamoja na zoezi hili kuongezwa siku, bado wananchi wanahitaji kuongozwa katika kujaza fomu na utaratibu mwingine ambao unafanyika kwa mara ya kwanza.
(PICHA: HARUNI SANCHAWA, GPL)