Na Mahmoud Zubeiry
MRISHO Khalfan Ngassa ameuzwa Simba kwa dau la Sh. Milioni 25 mchana wa leo, Azam imethibitisha.
Habari za ndani kutoka Azam, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka klabu hiyo, zimesema kwamba Simba wamelipa fedha hizo na wamesainiwa fomu za uhamisho na sasa Mrisho anafuata nyayo za baba yake Khalfan Ngassa, ambaye aliichezea Simba SC 1991/1992.
Azam ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya mchezaji huyo iliyemsajili kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya Yanga baada ya kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Na uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim Bakhresa mwenyewe, ambaye alikerwa na kitendo hicho akawaagiza wanawe, Wakurugenzi wa bodi ya timu wamuuze mchezaji huyo popote, haraka iwezekanavyo.
Meneja wa Azam, Patrick Kahemele amesema kamati ya ufundi ya klabu pamoja na uongozi walikubalina kumuweka sokoni Mrisho Ngassa mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Kagame Cup.
"Klabu iliamua kumweka sokoni Ngassa mara tu baada ya michuano ya Kagame kumalizika, kwa kuwa mwenyewe alionesha nia ya kujiunga na klabu yake ya zamani Yanga, sisi tuliwapa kipaumbele Yanga, lakini pia Simba nayo ilionesha nia ya kumtaka. Tukafungua bid na kutangaza tunahitaji $50,000. Yanga baada ya kuwajulisha juu ya hili wakatuma ofa ya millioni 20, Simba nao wakatuma millioni 25. Ofa zote zilikuwa chini ya kiasi tulichohitaji lakini baada ya majadiliano ya viongozi wote wa Azam tukaona bora tumuuze tu, kwa bei ya millioni 25.
"Kwa kuwa Simba walikuwa wameshafikia viwango na sisi lengo letu lilikuwa ni kumuuza Yanga, asubuhi ya leo tukawatumia email Yanga tukiwaambia waboreshe ofa yao na tukawaambia bid ya Ngassa itafungwa saa saba mchana, lakini hadi muda huo unafika Yanga hawakuwa wametujibu chochote, kitendo ambacho tulikitafsiri hawana nia ya dhati ya kumsaini mchezaji huyo, kwa upande mwingine Simba walikuwa tayari wamefikia dau tulilolitaka hivyo tukafunga bid na kumuuza mchezaji huyo kwa Simba," alimaliza Patrick.
Ngassa alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake aliosaini na Azam FC, akitokea Yanga miaka miwili iliyoipita kwa dau la Sh. Milioni 55, lakini wasiwasi unakuja kwamba, Ngassa ana mapenzi na Yanga na kwa Simba kumsajili, kuna hatari yaliyotokea akiwa Azam, yatajirudia hata akiwa kwa Wekundu wa Msimbazi.
Mapema leo mchana, Stewart Hall, kocha Muingereza wa Azam FC jana alifukuzwa katika klabu hiyo kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Habari ambazo BIN ZUBEIRY ilizipata kutoka ndani ya Azam, zilisema kwamba kikao cha jana cha pamoja baina ya Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC, Mwanasheria wa kampuni na kocha Stewart kimeafiki kuvunja ndoa hiyo na sasa Azam FC itakuwa chini ya kocha kutoka India, Vivek Nagul ambaye alikuwa anafundisha timu ya vijana.
Habari zinasema kwamba, mapema baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kagame, kati ya Azam na AS Vita ya DRC, Stewart aliitwa na kuambiwa asimtumie tena Ngassa kwa kitendo cha mchezaji huyo kwenda kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga, baada ya kufunga bao la ushindi.
Lakini Stewart katika kikao hicho, kwanza alimtetea Ngassa kutokana na kufunga bao la ushindi na kumuelezea kama mchezaji muhimu kwake, lakini msimamo wa bodi ulikuwa ni asipangwe tena.
Katika fainali, Stewart alimvalisha jezi Ngassa akamuanzishia benchi, lakini kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali alimuingiza kipindi cha pili timu ikiwa nyuma kwa 1-0 na mwisho wa mchezo ikashinda 2-1 yeye akifunga la pili, dhidi ya Yanga pia alimuingiza timu ikiwa nyuma kwa 1-0.
Lakini Ngassa alishindwa kurudia kile alichofanya kwenye mechi na AS Vita na Yanga ikashinda 2-0.
Mbali na Ngassa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ pia yuko katika wakati mgumu na jana inadaiwa alionekana akilia wakati anazungumza na kiongozi mmoja wa Azam, akiuliza ni lipi kosa lake.
Sure Boy, ambaye ni mtoto wa kocha wa timu ya vijana ya Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ jana hajafanya mazoezi na leo pia, naye pia akituhumiwa kucheza kinazi katika mechi dhidi ya Yanga.
Stewart anakuwa kocha wa nne ndani ya miaka minne kufukuzwa Azam, tangu Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini ni Stewart angalau anaacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame mwezi uliopita.
via BongoStaz.blogspot.com

Kauli ya Ngassa - Mwajiri wangu bado hajanipa taarifa rasmi juu ya suala hili
Muda mchache uliopita tumefanikiwa kufanya mazungumzo na mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa ambaye klabu yake Azam leo imethibitisha kwamba ameuzwa kwenda klabu ya Simba.
Katika mazungumzo hayo Mrisho Ngassa amesema kwamba yeye binafsi hajapata taarifa rasmi kutoka kwa klabu yake ya Azam juu ya kuuzwa kwenda Simba. "Kiukweli hizo taarifa mie nazisikia na kusoma kwenye mitandao tofauti lakini muajiri wangu bado hajanipa taarifa rasmi juu ya hili suala. Pia huu utaratibu sidhani kama ni sahihi, wanawezaje kuniuza timu nyingine bila kunihusisha, vipi kuhusu maslahi yangu katika hiyo timu nyingine nani ameyasimamia? Kwa maana hii bado nashindwa kuamini kama Azam watakuwa wamefanya hivyo. Ilipaswa wanipe taarifa kwamba Ngassa tunakuuza kwenda timu fulani na nina haki ya kuchagua kukubali au kukataa.
Ngassa akaendelea alivyoondoka Yanga, "Mimi sitaki kuondoka Azam huku kukiwa kuna hali ya kutokuelewana kati yangu na wao pamoja na wapenzi na mshabiki wa klabu hiyo ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye kipindi chote nilichokaa pale. Unaweza ukajiuliza kwanini mimi mpaka leo kwanini mashabiki wa Yanga wanaonyesha mapenzi kwangu au ninakuwa na ukaribu nao, ni kwa sababu wakati naondoka Yanga nilipewa baraka zote na klabu yangu, yaani niliondoka vizuri. Azam walikuja wakaongea na Yanga wakakubaliana na ada ya uhamisho then na mie nikapewa taarifa nikakaa chini na Azam tukakubalina mahitaji yangu binafsi sasa iweje leo wao wameshindwa kufuata utaratibu ule ule ambao waliufuata wakati wa kuninunua kutoka Yanga. Ilipaswa wao kabla ya kukubaliana na Simba ingebidi na mie nipewe taarifa ili kuweza kukubaliana mahitaji yangu binafsi na Simba then ndio niuzwe. lakini sivyo walivyofanya."
Alipoulizwa kama Simba wakimpa vile anavyovitaka atakuwa tayari kuichezea klabu hiyo, Ngassa alijibu, "Mpira ni kazi yangu, ninafanya hii kazi ili kuweza kujikimu kimaisha maisha. Kama klabu yoyote ikikubali kunipa mahitaji yangu niyatakayo na nikapendezewa nayo nitajiunga nayo. Simba ni klabu kubwa na nzuri yenye heshima kubwa kama ilivyo Azam na Yanga pia. Niliondoka Yanga baada ya kupewa maslahi mazuri na Azam, na kama Simba watanipa maslahi mazuri bila shaka nitakuwa sina pingamizi lolote, lakini ninachosisistiza taratibu zifuatwe na sio kunifanya mimi kiroba kunipeleka popote watakapo bila kunisikiliza mimi nataka nini."
By Aidan Charlie
ShaffiDauda.com