Wednesday, August 22, 2012

ZAIDI YA TANI TATU NA NUSU ZA BANGI ZACHOMWA MOTO JIJINI ARUSHA



 
Zaidi ya tani tatu na nusu ya madawa ya kulevya aina ya bangi yameteketezwa na jeshi la polisi mkoani Arusha katika kukamilisha operesheni ya kupambana na uhalifu na madawa ya kulevya inayoendelea mkoani hapa kwa mujibu wa mrakibu wa polisi na kaimu kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa Zuberi Mombeji alisema kuwa zoezi hilo ni endelevu na kuwataka wananchi mkoani hapa kutoa ushirikiano katika kutokomeza vitendo vya kihalifu.
 
Baadhi ya maofisa wa polisi akiwemo msemaji wa jeshi hilo mkoani hapa Rashid Nchimbi wakiangalia zoezi hilo likiendelea kwenye sehemu wanaochomea madawa hayo eneo la FFU nje kidogo ya jiji la Arusha.Picha na Mahmoud Ahmad,Arusha.