Steven
Kiprotich wa Uganda amekishangaza kikosi kikali cha Wakenya na kushinda
mbio za marathon kunako siku ya kuhitimisha michezo ya Olimpiki ya
London 2012.
Medali
hii ya dhahabu kwenye mashindano ya mwaka huu ni ya pili kwa Uganda
tangu mwaka 1972 marehemu John Akii Bua aliposhinda mbio za mita 400
kuruka viunzi kwenye mashindano ya Munich.
Kiprotich
ameshinda mbio hizi katika mda wa saa 2 dakika 08 na sekunde 01 kupitia
mitaa ya jiji la London akiwa mbele ya mshindi wa mara mbili wa mbio za
marathon na bingwa mtetezi Abel Kirui aliyemaliza wa pili katika mda wa
saa 2 dakika 08 na sekunde 27.
Mkenya
mwingine aliyeongoza mbio za leo kwa kipindi kirefu Wilson Kipsang,
ameshinda medali ya shaba akimaliza katika mda wa saa 2:09.37.
Hii
ni medali ya pili ya dhahabu kwa Uganda kwenye mashindano ya Olimpiki
baada ya miaka 40. Medali nyingine ya mashindano ya Olimpiki ilikua ya
fedha mkimbiaji wa mbio za mita 400 Davis Kamoga alipofukuzana na bingwa
wa nyakati hizo Michael Johnson wa Marekani mwaka 1996.
Mbio
hizi kwa kipindi cha kilomita 10 kilitawaliwa na Franck De Almeida
kutoka Brazil ikiashiria mbio kali zitakazowaniwa kati ya Wakenya na
Waethiopia. Lakini mbinu za Ethiopia zilichachuka pale Dino Sefir
alipoonekana kuishiwa nguvu na kasi yake kupungua na Kipsang kuanza
kuwasha moto na kuongoza kupitia mitaa kadhaa ya Jiji.
Mkenya
huyu aliweka pengo la sekunde 30 kupitia eneo ambalo lina vivutio safi
vya mji wa London na kufikia kituo cha kilomita 30 mwanariadha wa pili
wa Ethiopia Getu Feleke akaonyesha dalili za kukata tamaa na kuonekana
kurudi nyuma.
Kufikia
eneo lilikua na watazamaji wengi sana Kiprotich akaongezea mafuta miguu
na kuanza kumkimbiza Kipsang akigawanya kikundi cha wakimbiaji waliokua
wakisaka nafasi nono za medali.
Hatua
yake ilisababisha kuwaamsha Wakenya, kwanza mshindi wa Marathon za
Dubai Ayele Abshero wa Ethiopia aliyepunguza pengo lililowekwa na
Kipsang hadi sekunde 11 na kufikia kilomita 25 walikua pamoja.
Hadi
kilomita 30 Abshero alianza kuona mwendo kua na uchungu na miguu mizito
na kuachwa nyuma kwa sekunde 36 na hata kupitwa na Marilson Dos Santos
wa Brazil.
Kundi
lililokua likiongoza kupitia sehemu iliyofunikwa ya soko la Leadenhall
kuingia hatua ya kilomita saba za mwisho, Wakenya walijitahidi kumuacha
Kiprotich.
Lakini
Kiprotich akiwaonelea wa Kenya walio mbele yake wakisinzia na kuweka
kasi yake juu na kuwapita kwenye hatua ya kilomita 32 na kuwashangaza
alipowaacha kwa tofauti ya mita 200.
Kiprotich,
ambaye alihamisha mazowezi yake katika eneo maarufu la mazowezi huko
Eldoret ambako amejiunga na bingwa wa zamani wa mbio za mita 5000 Eliud
Kipchoge, aliongezea kasi yake na kudhibiti nafasi yake mbele.
Kupitia
kilomita mbili za mwisho, Mganda huyo mwenye umri wa miaka 23 alikua
mbele ya Kirui kwa tofauti ya sekunde 20 na aliweza kupata mda wa
kuchungulia anayemfuta yuko wapi kabla ya kunyakua bendera ya Uganda
kwenye hatua yake ya mwisho akiingia Mall, pembezuni mwa Kasri ya
Buckingham, na kuivaa shingoni wakati akivuka mstari wa kumalizia mbio
hizi.
Kumaliza mbio
1 Kiprotich UGA 2:08:01 - Dhahabu
2 Kirui KEN 2:08:27 - Fedha
3 Kiprotich KEN 2:09:37 - Shaba
1 Kiprotich UGA 2:08:01 - Dhahabu
2 Kirui KEN 2:08:27 - Fedha
3 Kiprotich KEN 2:09:37 - Shaba