Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema akiunguruma kwenye uzinduzi wa matawi katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwasili kwenye Uwanja wa Kwa Mbombe katika kijiji cha Madizini, Kata ya Mtibwa mkoani Morogoro ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Opereshi Sangara
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema amefungua matawi katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha
Katika ziara hiyo, Lema aliambatana na Mbunge wa Arumeru Masariki Mh Joshua Nassari(wa pili kulia) pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM kabla ya kujiengua na kujiunga na Chadema mapema mwezi Aprili mwaka huu, Ndg James Ole Millya, ambao nao kwa nyakati tofauti walipata fursa ya kuzunumza.
Mbali na suala la uzinduzi na upokeaji wanachama wapya, Lema alifanya harambee ya kukusanya fedha kusaidia shughuli za chama hicho katika Kata hiyo ambapo jumla ya Sh 219,500 zilichangwa na wananchi.
Akiondoka eneo hilo, Lema alilazimika kuwatuliza mamia ya watu waliokuwa wanafuatilia msafara wake ili kuepusha kutokea mwanya kwa watu wenye nia mbaya kuleta vurugu na uharibifu wa mali. Baadae msafara wake ulikatiza mitaa ya Stand Kuu ya mabasi makubwa na kisha kuelekea bustani ya City Park huku njiani akishangiliwa sana na baadhi ya watu wakinyoosha vidole kama ishara ya ushindi.
Wanachama wapya aliojiunga na chadema wakigombania kadi za chama hicho
Jitihada za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za kuwafikia wanachi ili kunadi sera zake, hususan katika mikutano inayoendelea katika mkoa wa Morogoro, zilikumbana na vikwazo mbali mbali katika baadhi ya maeneo, kama inavyoonyesha pichani, mtaro uliochimbwa katika barabara ya kuingia kijiji cha Namgezi kitongoji cha Kambi ya Keya jimbo la Ulanga Mashariki, kwa lengo la kuzuia magari yasipite.Picha na Joseph Senga