Gari hilo likiwa mtaroni baada ya kupinduka.
Mwili wa mtoto ukiwa umenasa kwenye gari.
...Mwili huo ukitolewa kwenye gari.
Gari likitolewa katika mtaro huo.
Mtoto aliyenusurika akimlilia mwenzake aliyefariki katika ajali hiyo.
Mtoto na dereva ambao wamenusurika katika ajali hiyo wakiwa na simanzi.
MTOTO
mmoja ambaye hakufahamika jina lake, amefariki dunia katika ajali ya
gari eneo la Kigamboni Machava leo wakati gari hilo likitokea Mji Mwema
kuelekea Kivukoni. Ajali hiyo imetokea baada ya gari hilo lenye namba za
usajili T 645 AVG kufunga breki ghafla kutokana na gari lililokuwa
mbele yake nalo kusimama ghafla hivyo kusababisha gari hilo kuingia
mtaroni na kupoteza uhai wa mtoto huyo.