Wednesday, August 22, 2012

MKUU WA WILAYA YA SERENGETI AFARIKI DUNIA



 
 Na Shomari Binda
            

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Kpteni mstaafu James Lyamungu amefariki Dunia leo mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa amesema ameshitushwa na taarifa ya kifo cha Mkuu huyo wa Wilaya ya Serengeti na kutoa pole kwa Wananchi wote wa Wilaya hiyo na Mkoa mzima wa Mara.

Amesema marehemu James Lyamungu alikuwa katika hali nzuri kiafya katika siku za hivi karibuni na alishirikia kikamilifu katika mbio za Mwenge wa Uhuru ulipowasili Mkoani Mara na kuanza mbio zake katika Wilaya ya Serengeti agosti 13 ukitokea Mkoani Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Mara amesema kabla ya kufikwa na mauti kwa mkuu huyo wa Wilaya katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili hii leo alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando tangu agosti 16 kabla ya kuhamishiwa katika hospitali hiyo agosti 21 na kufikwa na mauti.

Ameema kufutia taarifa za kifo cha Mkuu huyo wa Wilaya ya Serengeti kapteni mstaafu James Lyamungu Mkoa unaendelea kufanya mawasiliano na viongozi wengine wa Serikali waliopo jijini Dar es Salaam kuhusiana na taratibu zaidi za msiba huo.