Tuesday, August 21, 2012

MANENO OSWALD AMDUNDA RASHID MATUMLA KWA POINT



  Bondia Maneno Oswald akitangazwa baada ya kumdunda Rashid Matumla.
 Matumla akisulubiwa jukwaani wakati wa mpambano huo.

MPAMBANO wa ndondi baina ya mabondia Maneno Oswald na Rashid Matumla ambao ulifanyika ukumbi wa maraha wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es Salaam, katika kuadhimisha sikukuu ya Idd el Fitr, ulishuhudia Oswald akimchakaza Matumla kwa pointi.

Mbali na mpambano huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kulikuwa pia na burudani za aina mbalimbali, likiwemo disko la watoto ambao pia walifurahia kuogelea katika bwawa maalum na michezo mingine mingi. Kwa upande wa muziki kulikuwa na shoo kali zilizofanywa na wanamuziki Juma Nature, Mwasiti Almasi, Estelinah Sanga ‘Linah’, Maunda Zorro na kundi zima la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na mfalme, Mzee Yusuf.

(Picha: Musa Mateja na Richard Bukos/GPL)