Klabu ya Uitaliano Inter Milan
inasema kua kundi la wawekezaji kutoka Uchina limejitokeza kua
wawekezaji wa pili kwa ukubwa wa kumiliki hisa za klabu hiyo.
Katika taarifa ya Internazionale Holding,kampuni
mama inayosimamia masuala yote yanayohusiana na klabu imesema kua kundi
hilo limetangaza kua litamiliki sehemu ya hisa lakini kwamba familia ya
Moratti itaendelea kumiliki sehmu kubwa ya biashara.
Taarifa hio imesema kua uwanja mpya utajengwa
chini ya ushirikiano na sehemu ya China Railway Construction ikitazamiwa
kukamilishwa mnamo mwaka 2017.
Klabu hio imetangaza kua Kamchi Li, Kenneth
Huang na Fabrizio Rindi wote watakua wakurugenzi kwenye bodi kutokana na
uwekezaji huu.
Inter ndio klabu ya hivi karubini kuvutia
wawekezaji kutoka barani Asia. Klabu ya jijini London na Ligi kuu ya
Premiership Queen's Park Rangers ina milikiwa na Tony Fernandes, huyu
akiwa mmiliki wa kampuni uya ndege baranoi Asia, Air Asia, baada ya
kukamilisha ununuzi wake mwaka jana.