KAYA 55
Wilayani Magu, mkoa wa Mwanza hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba
zao zaidi ya 90 kubomolewa kisha kuchomwa ikiwa ni sehemu ya kutimiza
amri ya serikali nyumba hizo kubomolewa kupisha eneo hilo linalotajwa
kuwa ni hifadhi ya taifa.
Tukio
hilo la kinyama linadaiwa kufanyika kuanzia tarehe 1 Agosti hadi Agosti
2 mwaka huu, ambapo zioezi hilo liliendeshwa chini ya usimamizi wa mkuu
mpya wa wilaya hiyo Jaquline Liana akishirikiana na jeshi la polisi wilayani humo.