Tuesday, July 24, 2012

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AMALIZA ZIARA YA KUTANGAZA UTALII NCHINI MAREKANI


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akihojiwa na mwanahabari Jena Fox kutoka jarida la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni.Katika mahojiano hayo Balozi Kagasheki alipata fursa ya kuelezea fursa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini kwa soko la Marekani.
   Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Sued Kagasheki akimkabidhi tuzo ya kinyago Bi. Jena Fox, mwanahabari kutoka Jarida maarufu la nchini Marekani la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni. Tuzo hii ilitolewa na Bodi ya Utalii nchini kufuatia uandishi mzuri wa makala mbalimbali za kutangaza ukanda wa utalii wa kusini  katika soko la Marekani 

1.       Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini Dk. Sloyce Nzuki akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Wageni cha Marekani (USTOA) Bi. Peggy Murphy mara baada ya kufanya nae mazungumzo juu ya namna ya kuongeza idadi ya wageni nchini kutoka Marekani jijini  new York.