Majeruhi wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi (4) wakisubiri kupewa matibabu katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kufikishwa hapo usiku huu wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga
Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali usiku wa leo na kuua watu watatu na kujeruhi 38Basi hilo kwa mbele
Majeruhi Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma akisubiri kupewa matibabu katika Hospitali ya mkoa wa Iringa
Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali usiku wa leo na kuua watu watatu na kujeruhi 38Basi hilo kwa mbele
Majeruhi Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma akisubiri kupewa matibabu katika Hospitali ya mkoa wa Iringa
Dereva wa basi hilo akifikishwa hospitali |
Ajali mbaya ya basi ya Tony Sley yenye namba za usajili T 218 ACH lililokuwa likitokea Tunduma mkoani Mbeya kwenda jijini D'Salaamimeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia na mmoja mtanzani huku watu 38 wakijeruhiwa .
Ajali hiyo imetokea katika eneo la kona za mlima wa kitonga kwenye barabara kuu ya Iringa –D'Salaam leo majira ya saa 12 za jioni baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa mbele yake .
Wakizungumza na mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilolo Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wao alisema Agnes Lukasi (30) .
Bi Agnesy alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo akifanya uzembe huyo walikuwawakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila mafanikio .
Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso .
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa aliuthibitishia mtandao huo kuwa jumla ya abiria 38 ndio waliojeruhiwa katika ajali hiyo.
Aliwataja baadhi ya majeruhi ambao majina yao yamepatikana na kulazwa katika hospital teuli ya mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Boyd Simwings(43) , Violet Chambale(35),Zilombo Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39), Mwamba Andrew (27) , Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote raia wa Zambia.
Wengine ni Martine Shombe( 29) mkazi wa Tunduma, Zainabu Amuri (32) mkazi wa D'Salaam , Efrain Mwampashi (31) mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi wa Tunduma, Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma, Mrashi Handu (38) mkazi wa Igulusi, Juma Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi wa Arusha, Muka Muka (26) mkazi wa Tunduma, Edina Ramadhan (3) mkaziwa Tunduma na Benjamin Enock (33) mkazi wa Mbeya
Wengine ni Agness Lukas (30) mkazi wa Tunduma , Dina Lukas (4) mkazi wa Tunduma Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi wa Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa Zambia pia.
Alisema majina ya majeruhi zaidi yatapatikana hivi karibuni baada ya majeruhi waliopo Hospital ya wilaya ya Kilolo Ilula kufika mjini Iringa .
Mbali ya majeruhi hao pia aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Cla Pily (32) na Dany Kawina (43) wote wafanyabiashara raiawa Zambia pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni mtanzania.
Kamanda Kamhanda mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya ajali hiyo bado aliwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha kwa uangalifu wa hali ya juu na kuwa jeshi lake mkoani Iringa halitalala kuwabana madereva wazembe.