Baadhi ya miili ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya Seagull.
Baadhi ya wasafiri waliookolewa katika ajali hiyo.
(Picha kwa hisani ya http://zanzibaryetu.wordpress.com/)
MIILI 25 ya watu walifariki katika ajali ya meli ya Seagull iliyozama jana imeokolewa kutoka majini. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar ilizama eneo la Chumbe jirani na Zanzizar. Watu 145 walionusurika katika ajali hiyo wameokolewa wakati watu 120 wakiwa bado hawajapatikana mpaka mwisho wa zoezi la uokoaji lililofungwa jana jioni baada ya giza kuingia. Seagull ilikuwa na abiria 250, watoto 31 na wafanyakazi 9 ikiwa ni jumla ya watu 290. Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni dhoruba kali iliyotokea baharini wakati chombo hicho kikiwa safarini. Zoezi la uokoaji litaendelea leo.