Sunday, July 29, 2012

Viti kadha vitupu kwenye Olimpiki

 29 Julai, 2012 - Saa 17:36 GMT

Kumezuka mabishano nchini Uingereza kuhusu viti vitupu kuonekana kwenye mashindano kadha ya Olimpiki siku ya Jumamosi, pamoja na mashindano ya beach volleyball, gymnastics na mashindano ya awali ya kuogelea.
Viti vitupu kwenye mechi ya tennis ya wanawake Jmamosi
Wakuu wa Olimpiki wanasema watachunguza.
Inafikiriwa viti hivo vitupu ni vile vilivotengwa kwa ajili ya wakuu, wafadhili, wanariadha na waandishi wa habari.
Mwandishi wa BBC anasema swala la tikiti ni tete, kwa sababu washabiki wengi wa Uingereza walitaka kununua tikiti wakaambiwa zimekwisha.

Source:BBC