Bendi ya Muziki "Ngoma Africa band" yenye makao Ujerumani,
Inatoa pole na rambi rambi kwa ndugu na jamaa wote waliopatwa
msiba kutokana na jali ya meli ya MV Skagit,iliyotokea jana 18-7-2012
jirani na Chumbi,Zanzibar.
Ngoma Africa Band inaungana na watanzania wote walio nyumbani na
nje ,katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa kitaifa,msiba huu ni wetu
sote. Katika maombelezo bendi inasimamisha shughuli zake kwa mda
wa wiki moja.
Mungu ibaraki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika