Sunday, July 22, 2012

NAPE ATUA KIGOMA, KUUNGURUMA UWANJA WA COMMUNITY CENTRE MWANGA MCHANA HUU

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kipampa mkoani Kigoma leo kwa ajili ya mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye Uwanja wa Comunity Centre, Mwanga mkoani humo. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na ujumbe wake wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kipampa mkoani Kigoma. Kushoto ni Waziri Steven Wasira.

Nape akiwasilimia viongozi wa CCM waliompokea Uwanja wa Ndege wa Kipampa, Kigoma leo.

Mbunge wa Kigoma mjini Peter Serukamba akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili na Nape kwenye Uwanja wa Ndege wa Kipampa mkoani humo leo.

Baadhi ya watu waliokuwa na shauku ya kumuona Nape wakichungulia kupitia uzio wa Uwanja wa ndege wa Kipampa mjini Kigoma.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akishiriki na vijana kucheza ngoma ya Kasimbo ya mkoa wa Kigoma, baada ya kuwasili Uwanja wa Kipampa mkoani humo, leo.

Waendesha pikipiki wakiongoza msafara wa Nape kutoka Uwanja wa Ndege wa Kipampa mkoani Kigoma leo.

(Picha zote na Bashir Nkoromo)