Sunday, July 22, 2012

MWENGINE KAZUA MAKUBWA :- KIJANA AFUMANIWA AKIMBAKA NG'OMBE WA JIRANI YAKE ZIZINI - MBEYA



Na Bosco Nyambege,Rungwe.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Tumsifu Mwambusi (20),mkazi na mkulima wa Kijiji cha Mwela,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amefumaniwa akimbaka ng'ombe.

Tukio hilo la ajabu yake limetokea Julai 15 mwaka huu majira ya saa mbili za usiku ambapo jamaa huyo alikwenda kwenye makazi ya Bwana Leonard Mwangwemba,kisha kuingia ndani ya zizi na kuanza kumbaka   ng'ombe huyo hali iliyopelekea ng'ombe huyo kuanza kupiga kelele kwa kuomba msaada. 

Ndipo wakazi wa eneo hilo walielekea eneo la tukio na kumkuta kijana huyo akiendelea na kitendo hicho na kumshushia kipigo cha mbwa mwizi mara baada ya kuvunja amri ya sita ya kuzini na ng'ombe huyo.

Aidha,kufuatia hali hiyo Kijana Mwambusi aliomba msamaha kwa kitendo hicho lakini wananchi hao hawakujali na mara akajikuta akimwagiwa maji ya baridi na kipigo kikiwa kinaendelea na kusababishiwa maumivu sehemu mbalimbali ya  mwili wake.

Hata hivyo wazazi wa kijana huyo walijaribu kutoa kiasi cha shilingi 100,000 kwa wananchi hao ili waweze kumwachia kijana wao kufuatia kipigo alichokuwa akipewa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Andongwisye Mwakalinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewasihi wananchi hususani vijana kumwomba mungu muda wote ili kuondokana na majaribu yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.