Wednesday, July 25, 2012

MNYAMA HOI KWA AZAM, APIGWA 3-1



Shujaa wa Azam FC, John Bocco akishangilia moja ya mabao aliyoifungia timu yake leo.


Wachezaji wa Azam wakishangilia ushindi wao.


Beki wa Simba, Lino Musombo (kulia) akichuana na Kipré Tchétché wa Azam.


Mashabiki wa Azam wakiwa na furaha.


Mashabiki wa Simba wakiwa hawaamini kilichotokea.


Shabiki wa Azam aliyekuwa kivutio uwanjani leo.

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo wameondolewa katika Michuano ya Kombe la Kagame baada ya kufungwa na Azam FC bao 3-1 katika Robo Fainali ya michuano hiyo iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam yote matatu yamefungwa na John Bocco wakati la Simba likifungwa na Shomari Kapombe.

(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)