Wednesday, July 18, 2012

Meli yazama Zanzibar

 18 Julai, 2012 - Saa 14:12 GMT

Habari za hivi punde

Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili imethibitiswha kuzama katika bahari ya hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar. Meli hiyo kwa jina SKAGIT ilikuwa inatoka Dar Es Salam kuelekea Zanzibar.

Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.

Jeshi la polisi la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mbia mbili wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar.

Itakumbukwa kwamba, ni takriban mwaka mmoja sasa tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.


Source: BBC