Wednesday, July 18, 2012

MABINGWA WA COPA COCA COLA WAPOKELEWA MKOANI MORO, WAFANYIWA SHEREHE


Mabingwa wa Copa Coca Cola wakiwa na kombe lao wakati wa mapokezi hayo.

Msafara wa mabingwa hao ukiwa katikati ya mji wa Morogoro.

Kikosi cha mabingwa wa Copa Coca Cola kikiwa katika pozi.

Vijana wa Moro wakiingia katika ukumbi wa 'The Highlands' kwa ajili ya sherehe.

Diwani wa Kata ya Kilakala, Ribbon Mkali 'Okwi' akimkaribisha mbunge wa jimbo la Morogoro, Aziz Abood  (kushoto) katika sherehe hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kushoto) akipokewa na Diwani wa Kata ya Kilakala, Ribbon Mkali' Okwi' ambaye sherehe hizo zilifanyika katika kata yake.

Nahodha wa timu ya Vijana ya mkoa wa Morogoro, Hassan Juma akimkabidhi kombe la ubingwa wa mashindano hayo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera.

 Joel Bendera akiwa na kombe hilo baada ya kukabidhiwa na vijana wake waliomtoa kimasomaso kwenye michuano hiyo iliyoshirikisha mikoa yote ya Tanzania.

Mfungaji Bora wa michuano hiyo kwa mwaka huu akiwa ametupia mabao10, Mutelemwa Albogast Katunzi (kulia) akiwa na Mchezaji Bora wa mwaka huu pia kutoka Morogoro, Shiza Kichuya wakipongezwa.

Katibu msaidizi wa chama cha soka mkoa wa Morogoro, Emmanuel Kimbawala akimtambulisha mchezaji bora wa michuano hiyo kwa mwaka jana, Miraji Adam Seleman 'TATA' . Miraji hakukuwemo kwenye kikosi cha mwaka huu kutokana na kuchaguliwa timu ya taifa ya vijana 'Serengeti Boys'.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Serengeti Boys ambao wametokea timu hiyo ya Morogoro, Basil Seif  (kulia) na Miraji Adam Seleman wakishirki kwenye sherehe hizo na wenzao. Mwaka jana Morogoro ilishika nafasi ya pili wakati Kigoma ikiibuka mabingwa.

Joel Bendera akimpongeza kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Mexime kwa kazi kubwa aliyoifanya.

---

MABINGWA wapya wa michuano la Copa Coca Cola, vijana wa mji kasoro bahari 'Morogoro' jana jioni walipokelewa kwa shangwe na kufananishwa na timu ya taifa ya Hispania kwa uchezaji wao mpaka mapokezi. 

Vijana hao waliibuka kidedea katika mashindano ya Copa Coca Cola 2012 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita jijijni Dar es Salaam kwa kuinyuka Mwanza kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliokuwa mkali na wakuvutia.

Baada ya mapokezi hayo, washindi hao walifanyiwa sherehe kwenye ukumbi wa mpya wa kisasa wa 'The Highlands' uliopo katika milima ya Ulugulu.

(PICHA ZOTE NA DUNSTAN SHEKIDELE/GPL, MOROGORO)