29 Julai, 2012 - Saa 16:41 GMT
Mbio za baiskeli Olimpiki
Mwakilishi wa Uholanzi kwenye
mashindano ya Olimpiki Marianne Vos aliondoa hisia za kosa kosa yake ya
miaka mingi iliyopita leo jumapili na kujinyakulia medali ya dhahabu kwa
kushinda mbio za barabarani na kuwaudhi mashabiki wa Uingereza kwa
kumpiku mwakilishi wao.
Vos, aliyemaliza wa pili katika mashindano ya
miaka mitano iliyopita baada ya ushindi aliopata mwaka 2006, alifyatuka
na kumuacha mwenziye wa karibu Lizzie Armitstead ambaye angalau
alimaliza kwa kushinda medali ya fedha.Baada ya mbio hizo Vos alisema, "mashindano ya Olimpiki ni tofauti na mashindano ya Dunia. Nilifahamu ni tofauti na mashindano ya Dunia.
Mrusi Olga Zabelinskaya, akiwa miongoni mwa waendesha baiskeli walioponyoka kundi kubwa kwenye umbali wa kilomita 140.3 alisema baada ya mbio zilizoanzia na kumalizika kwenye Mall iliyo katikati mwa jiji la London aliwambia wandishi wa habari kuwa, nimeridhika kuchukua uwamuzi wa kujikwamua kutoka kundi kubwa. Kwa sababu tulijifunza baada ya kuangalia mbio za wanaume jana. Kwa hiyo lilikua funzo kwetu.
Bingwa mtetezi wa mbio hizi, Muingereza Nicole Cook hakuonyesha umakinifu na nguvu yake ya kawaida akishindwa kufikia kasi aliyoiweka mshindi Vos.
Source: BBC