Tuesday, July 24, 2012

Mabasi ya Dar Express, Simba Mtoto yamegongana uso kwa uso eneo la Wami


Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na basi la Simba Mtoto lililokuwa linaenda Tanga yamegongana uso kwa uso maeneo ya Wami. Mwanahabari wa "Globu ya Jamii" aliyekuwa eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna maafa ya watu kupoteza uhai yaliyoropotiwa ila, watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado hakijafahamika. 

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Chalinze.

Picture
Abiria wa wakishushwa kupitia madirishani
Picture
Abiria wakijaribu kumwokoa mwenzao aliyenaswa
Picture
Abiria wakiendelea na juhudi za kuwatoa wenzao
picha na taarifa via IssaMichuzi.blogspot.com