Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali
Felix Samillan akisalimiana na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani
Dodoma, Omar Kariati wakati wa hafla ya wakulima wa kata hiyo
kukabidhiwa matrekta manne kwenye Ofisi za Suma JKT, Mwenge Dar es
Salaam, leo. Julai 26, 2012.
Diwani Kata ya Kwadelo Kondoa mkoani
Dodoma Alhaji Omar Kariati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
hafla ya wakulima wa kata hiyo kukabidhiwa matrekta manne kwenye Ofisi
za Suma JKT, Mwenge Dar es Salaam, leo. Julai 26, 2012.
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji
Omari Kariati (wa tatu kushoto) akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata
hiyo, Abdallah Ramadhani (kushoto), Gabriel Galahenga, baada ya
kuwakabidhi wakulima hao matrekta manne, kwenye Ofisi za Shirika la
Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es
Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta
hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni
hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja ambayo inauzwa kwa sh.
milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na
kisha kulipa zilizobaki katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa
diwani huyo.
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji
Omari Kariati, akimkabidhi funguo za trekta, mkulima wa Kata hiyo,
Abdallah Ramadhani, katika hafla ya diwani huyo kukabidhi matrekta manne
wakulima kutoka kata hiyo, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai
26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata
hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa
diwani Kariati. Trekta moja ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima
hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa zilizobaki
katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo. Wengine, ni
wakulima wa kata hiyo ya Kwadelo, Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga
(wapili kushoto) na Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan.
Mkulima wa Kwadelo, Kondoa mkoani
Dodoma, Gaberiel Galahenga akimkabidhi barua Diwani wa Kata hiyo, Omari
Kariatikwa ajili ya diwani huyo kumpelekea kama shukurani Mkuu wa JKT,
kwa shirika la Suma JKT kuwawezesha wakulima wa kata hiyo kukubali
kuwapa mattekta wakulima wa kata hiyo kwa nusu ya bei na kisha kumalizia
pole pole. Wengine katika picha ni, Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga
(watatu kushoto) na Meneja wa Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan.